1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiEthiopia

Idadi ya vifo vya maporomoko ya ardhi Ethiopia yafikia 299

24 Julai 2024

Idadi ya vifo kutokana na maporomoko ya ardhi Ethiopia imepanda hadi watu 229. Serikali imesema idadi hiyo huenda ikaongezeka zaidi huku shughuli ya kuwatafuta manusura na waliokufa ikiendelea katika siku ya pili.

https://p.dw.com/p/4ieKQ
Shughuli za uokozi na utafutaji maiti zaendelea Gofa Zone
Tukio hilo lilitokea katika eneo la Gofa Zone kusini mwa Ethiopia kufuatia mvua kubwaPicha: Gofa Zone Government Communication Affairs Department

Maporomoko hayo ya ardhi yalisababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika eneo la Gofa Zone Jumapili na Jumatatu. Idara ya Mawasiliano ya Gofa Zone ilisema wanaume 148 na wanawake 81 ni miongoni mwa waliokufa. Imeongeza kuwa zoezi la utafutaji linaendelea kwa kasi.

Picha ziliwaonesha watu wakichimba kwenye tope kwa kutumia mikono. Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema vifo hivyo vimemhuzunisha sana. Mkuu wa Shirika la Afya Duniani - WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye ni Muethiopia, ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizoathirika na akaongeza kuwa timu ya WHO imetumwa katika eneo la mkasa huo ili kutoa mahitaji ya dharura.