Waliokufa kufuatia maporomoko ya ardhi Ethiopia yafikia 157
23 Julai 2024Matangazo
Idadi ya vifo vilivyotokana na matukio mawili ya maporomoko ya ardhi kusini mwa Ethiopia vimeongezeka kwa kasi hadi 157 na serikali ikisema idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi.
Taarifa ya serikali inasema maporomoko ya ardhi yamefukia watu katika eneo la Gofa Kusini mwa Ethiopia, na katika pirika za uokozi lilitokea lingine katika eneo hilohilo na kuwakumba walokuwa wakitoa msaada.
Mkuu wa Wakala wa Kitaifa wa Kukabiliana na Maafa katika Kanda ya Gofa, Markos Melese, amesema kazi ya kutafuta manusura na miili ya waiokufa bado inaendelea. Na kuongeza kuwa eneo hilo lina changamoto nyingi sana.
Taarifa rasmi kutoka katika eneo hilo alisema takribani watu 50 wamekufa na kwamba watoto na maafisa wa polisi ni miongoni mwa waliopoteza maisha.