1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo kutokana na lori la mafuta Uganda vyapanda hadi watu 15

23 Oktoba 2024

Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa lori la mafuta nchini Uganda imepanda hadi watu 15. Polisi imesema leo kuwa watu wengine wanne wamefariki kutokana na majeraha waliyoyapata.

https://p.dw.com/p/4m99U
Nigeria City Majiya | Lori la kubebea mizigo lililolipuka
Moshi uliotokana na moto mkubwa baada ya lori la mafuta kupinduka na kulipuka, huko Majia, Jimbo la Jigawa, Nigeria, Oktoba 16, 2024.Picha: UGC/Social Media/REUTERS

Msemaji wa polisi mjini Kampala Patrick Onyango amesema watu 25 walijeruhiwa katika mkasa huo na wamelazwa hospitali, wengine wakiwa na majeraha mabaya ya kuungua. Polisi imesema mchakato unaoendelea wa kuwatambua waliokufa ni mgumu kwa sababu wengi wa waathiriwa waliungua kiasi cha kutotambulika. Lori hiyo ililikuwa ikisafiri kutoka Kampala kwenda Gulu kaskazini mwa Uganda wakati ilipobingiria na kuwaka moto jana alasiri katika mji wa Kigogwa, karibu kilometa 25 kaskazini mwa mji mkuu. Mnamo mwaka wa 2019, watu 19 walikufa wakati lori ya mafuta ilipoyabamiza magari mengine kaskazini mwa nchi hiyo na kulipuka.