1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na Haki

ICJ yasema ina mamlaka kesi ya Ukraine dhidi ya Urusi

3 Februari 2024

Mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa ICJ, imesema jana kuwa inayo mamlaka ya kuamua kuhusu ombi lililowasilishwa na Ukraine kuitaka itoe tangazo kwamba Kyiv haihusiki na mauaji ya kimbari.

https://p.dw.com/p/4bzmQ
The Hague | Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ.
ICJ ni mahakam ya juu ya Umoja wa Mataifa.Picha: REMKO DE WAAL/ANP/AFP

Mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa ICJ, imesema jana kuwa inayo mamlaka ya kuamua kuhusu ombi lililowasilishwa na Ukraine kuitaka itoe tangazo kwamba Kyiv haihusiki na mauaji ya kimbari, lakini siyo juu ya vipengele vingine vya kesi ya Ukraine dhidi ya Urusi.

Ukraine ilifugua kesi hiyo siku chache tu baada ya Urusi kuanzisha uvamizi dhidi yake Februari 2022, ikidai kuwa Moscow ilitumia madai ya uongo ya mauaji ya kimbari kuhalalisha uvamizi huo.

Soma pia: ICJ kutangaza uwezo wake katika kesi ya kuvamiwa Ukraine

Lakini mahakama hiyo imesema haitatoa hukumu kuhusu suala hilo, na badala yake itaamua juu ya iwapo Ukraine ilikiuka mkataba wa kuzuwia mauaji ya kimbari, kama ilivyodaiwa na Rais wa Urusi Vladmir Putin kuhalalisha uvamizi huo.

Hukumu ya mwisho inatazamiwa kuchukuwa miaka kadhaa.