1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

HRW: Mamlaka za Tunisia zawakandamiza wanaompinga rais

20 Agosti 2024

Msemaji wa shirika la kutetea haki, Human Rights Watch Bassam Khawaja amesema mamlaka nchini Tunisia imezidisha ukandamizaji kwa wanaomkosoa Rais Kais Saied.

https://p.dw.com/p/4jhiY
Tunisia | Rais Kais Saied
Utawala wa Rais wa Kais Saied unashutumiwa kwa kuwakandamiza wapinzani na wanaharakati wanaompinga Rais Picha: Chokri Mahjoub/ZUMA Wire/IMAGO

Human Rights Watch imesema hayo huku ukiwa umebakia muda wa zaidi ya wiki sita kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais nchini humo.

Human Rights Watch katika ripoti yake imesema serikali imewafunga makumi ya wapinzani na wanaharakati mashuhuri.

Khawaja ameongeza kusema kwamba mamlaka ya Tunisia imewaondoa karibu wagombea wote wakuu kutoka kwenye kinyang'anyiro cha urais na hivyo uchaguzi huo umebaki kuwa kama ni utaratibu wa kawaida tu.

Viongozi mashuhuri wa upinzani, wanaharakati, waandishi wa habari wamekamatwa na kutiwa ndani miongoni mwao ni bibi Abir Moussi, mkosoaji mkubwa wa rais Kais Saied.