Hamas na Fatah wakaribia makubaliano ya mtawala wa Gaza
4 Desemba 2024Matangazo
Afisa mmoja wa Mamlaka ya Palestina amethibitisha kwamba makubaliano ya awali yamefikiwa baada ya wiki kadhaa za mazungumzo mjini Cairo. Amesema kamati hiyo inaweza kuwa na wajumbe 12 hadi15, wengi wao kutoka Gaza.Kamati hiyo huenda ikauhitimisha utawala wa Hamas na pengine kusaidia kuendeleza mazungumzo ya kusitisha mapigano na Israel. Pande hizo hasimu zimefanya majaribio kadhaa ya upatanisho ambayo hata hivyo hayakuzaa matunda, tangu Hamas ilipochukua mamlaka huko Gaza mwaka 2007. Israel hata hivyo imeondoa uwezekano wa makundi hayo mawili kuitawala Palestina, inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi.