Matangazo
Inaelezwa kuwa vibanda vya biashara na baadhi ya maeneo ya ibada ukiwemo msikiti mmoja na kanisa la PCEA yamechomwa moto na magenge ya wahalifu.
Kwengineko katika Kaunti ya Kiambu, magenge ya wahalifu walivamia shamba la Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta na kuiba mifugo.
Je, maandamano ya jana Jumatatu yamekuwa na athari ya kiasi gani nchini Kenya? Babu Abdallah anazungunza na mchambuzi wa siasa akiwa mjini Nairobi, Martin Oloo.