1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali mbaya ya hewa yaathiri shughuli za ndege Ujerumani

5 Januari 2025

Safari kadhaa za ndege kwenye viwanja vitatu nchini Ujerumani vya miji ya Frankfurt, Munich na Stuttgart zimefutwa kutokana na hali mbaya ya hewa ya baridi kali.

https://p.dw.com/p/4opbv
Ujerumani| Lufthansa
Hali mbaya ya hewa imepelekea kukatishwa kwa safari za ndege katika baadhi ya viwanja vya ndege UjerumaniPicha: Matthias Schrader/AP/dpa/picture alliance

Safari kadhaa za ndege kwenye viwanja vitatu nchini Ujerumani vya miji ya Frankfurt, Munich na Stuttgart zimefutwa kutokana na hali mbaya ya hewa ya baridi kali. Tahadhari ya mvua kubwa na kuanguka theluji ndiyo chanzo cha kutatizika kwa shughuli za usafiri huo wa anga leo Jumapili

Tovuti ya Uwanja wa Ndege wa Frankfurt ilionya kuhusu hali mbaya ya hewa na kuwashauri wasafiri kuangalia hali ya safari zao za ndege kabla ya kuelekea uwanja wa ndege.

Soma zaidi. Baerbock: EU inaendelea kufuatilia mchakato wa kisiasa Syria

Uwanja wa ndege mjini Munich pia kupitia tovuti yake mapema leo uliandika kwamba safari nyingi za ndege huenda zingefutwa kwa sababu ya utabiri wa hali mbaya ya hewa.

Shirika la Reli la Taifa la Ujerumani Deutsche Bahn (DB), nalo pia limetoa tahadhari kwamba hali mbaya ya hewa inaweza kuathiri shughuli zake.