SiasaUrusi
Urusi yakataa azma ya Ujerumani kupata kiti cha kudumu UN
3 Januari 2025Matangazo
Nebenzya amesema iwapo baraza hilo lingefanyiwa mageuzi, baadhi ya nchi kamwe haziwezi kuwa wanachama wa kudumu, hata ikiwa zingetamani kufanya hivyo.
Amesema anazungumzia hasa kuhusu Ujerumani na Japan. Madajiliano kuhusu mageuzi katika Baraza la Usalama yamekuwa yakiendelea kwa miaka mingi ndani ya Umoja wa Mataifa.
India na nchi za Afrika zina matumaini ya kupata kiti cha kudumu katika baraza hilo. Hata hivyo, kwa muda mrefu serikali ya Ujerumani nayo imekuwa na azma hiyo.