Haiti yakubali kupokea kikosi cha askari wa Kenya
31 Julai 2023Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Haiti, Jean Victor Geneus, ilisema kuwa Haiti inathamini nia ya mshikamano wa Afrika na inatazamia kuukaribisha ujumbe unaopendekezwa na Kenya.
Kenya ilitangaza siku ya Jumamosi (Julai 29) kuwa ilikuwa tayari kupeleka maafisa 1,000 wa polisi ili kusaidia kutoa mafunzo na msaada kwa wenzao wa Haiti katika kupambana na magenge ya wahalifu ambayo yamechukua udhibiti wa sehemu kubwa ya mji mkuu, Port-au-Prince.
Soma zaidi: Kenya iko tayari kupeleka kikosi kusaidia kurejesha utulivu Haiti
Guterres atolea wito jamii ya kimataifa kuisaidia Haiti
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Kenya, Alfred Mutua, alisema Kenya ingeliutuma ujumbe wa kutathmini hali ilivyo nchini Haiti katika wiki chache zijazo.
Pendekezo hilo la kuisaidia Haiti bado linatakiwa kukubaliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuidhinishwa na mamlaka za ndani.