Guterrs: Tuongezeni juhudi kukabili mabadiliko ya tabia nchi
28 Novemba 2023Guterres ametahadharisha kuwa "dunia imenaswa katika mzungumko mbaya" na kuwahimiza viongozi kuchukua hatua ili kudhibiti ongezeko la joto hadi nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha Celcius na kuacha kutumia nishati ya visukuku.
Soma pia:Guterres ataka mkutano wa COP28 utumike kuinusuru dunia
Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameyasema hayo kuelekea mkutano wa COP28 ambapo watu 70,000 wanatarajiwa kuhudhuria mkusanyiko mkubwa zaidi kuwahi kutokea wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa.
Wapatanishi wa kitaifa katika mkutano huo watakabiliana na masuala kadhaa ikiwemo mustakabali wa nishati ya visukuku, usaidizi wa kifedha kutoka kwa mataifa tajiri wachafuzi wa mazingira kwenda kwa mataifa masikini yanayoathirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa.