MigogoroSudan
Guterres atahadharisha kuhusu ongezeko la machafuko Sudan
26 Septemba 2024Matangazo
Taarifa ya Umoja wa Mataifa kuhusu mkutano kati ya Guterres na Jenerali Abdel-Fatah Al-Burhan imesema katibu mkuu huyo ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu machafuko yanayoongezeka Sudan.
Soma pia: Marekani kutoa msaada zaidi wa dola milioni 424 kwa Sudan
Machafuko hayo yanatajwa kuendelea kuwa na athari kubwa kwa raia wa Sudan na kuna hatari ya machafuko hayo kuenea katika ukanda huo.
Afisa Mkuu wa uratibu wa misaada wa Umoja wa Mataifa Joyce Msuya amesema watu nchini Sudan wamevumilia miezi 17 ya hali ngumu na mateso yanaendelea.