Greta Thunberg ajiunga na maandamano ya tabianchi Uholanzi
12 Novemba 2023Maandamano hayo yanafanyika ikiwa ni siku kumi kabla ya uchaguzi mkuu nchini Uholanzi. Waandaaji wamesema maelfu ya watu wanashiriki maandamano hayo.
Utafiti unaonesha kwamba masuala muhimu yanayopewa kipaumbele katika kampeini ya uchaguzi ni mgogoro wa ukosefu wa makaazi nchini humo,viwango vya hali ya maisha pamoja na uhamiaji.
Soma zaidi: Wanaharakati wa hali ya hewa waanza maandamano makubwa
Kwa mujibu wa utafiti wa maoni uliofanywa na taasisi ya I&O suala la mabadiliko ya tabia nchi sasa halipewi umuhimu kama ilivyoshuhudiwa katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2021 nchini humo.
Utafiti wa maoni ya wapiga kura pia umeonesha uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na mpambano mkali kati ya chama cha siasa za wastani za mrengo wa kati,VVD cha waziri mkuu anayeondoka Mark Rutte na chama kipya cha NSC kinachoongozwa na Pieter Omtzigt kiongozi wa mapambano dhidi ya ufisadi.