Ujerumani kupeleka meli za kivita Indo-Pasifik
4 Juni 2023Hatua hiyo ni kutokana na mvutano unaoongezeka kati ya China naTaiwanna pia kutokana na mgogoro wa bahari ya kusini mwa China.
Akizungumza katika mkutano wa usalama wa eneom la Asia unaofanyika Singapore, waziri Pistorius amesema nchi zinahitaji kusimamia sheria kwa mujibu wa utaratibu wa kimataifa pamoja na kuhakikisha ulinzi wa njia kuu za baharini.
Soma pia:China: Ujerumani yatakiwa kuunga mkono muungano wa China na Taiwan
China inadai karibu bahari yote ya kusini mwa nchi hiyo ni yake, licha ya mahakama ya kimataifa kutoa uamuzi kwamba madai ya Beijing hayazingatii msingi wa kisheria.
Wakati huo huo China imejenga vituo vya kijeshi kwenye visiwa vyenye utajiri wa gesi na maeneo ya kuvua yaliyo na viumbe wa majini wengi.
Ujerumani imebanwa kati ya hatua za kulinda usalama na maslahi ya uchumi wake kutokana na kwamba China ni mshirika muhimu wa kibiashara wa Ujerumani. Asilimia 40 ya biashara ya nje ya Ulaya inapitia kwenye bahari ya kusini ya China.