1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatakiwa kuunga mkono muungano wa China na Taiwan

Daniel Gakuba
15 Aprili 2023

China imetumia ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock mjini Beijing, kuitaka Ujerumani iunge mkono mchakato wa amani wa China kuungana na Taiwan

https://p.dw.com/p/4Q8b0
China Aussenministerin Annalena Baerbock | Wang Yi
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock (kushoto) na mwenzake wa China Wang Yi mjini BeijingPicha: Soeren Stache/dpa/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema nchi yake inatumai kuwa Ujerumani itaunga mkono mchakato wa amani wa kuiunganisha Taiwan na China, akisema katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake miaka ya nyuma China iliunga mkono kuungana kwa Ujerumani kama nchi moja.

Hayo yameelezwa kufuatia ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock nchini China, ambayo imehitimishwa leo. Hapo jana, Waziri Baerbock alionya kuwa jaribio lolote la China kuidhibiti Taiwan halitakubalika, na litakuwa na athari mbaya kwa Ulaya.

China ambayo huichukulia Taiwan kama sehemu ya himaya yake, imesema hairuhusu mataifa ya kigeni kuingilia katika masuala ya ndani ya China.

Baada ya ziara yake nchini China, Waziri Baerbock ameelekea nchini Korea Kusini, ambapo amezuru sehemu yenye ulinzi mkali inayoitenganisha Korea Kusini na Korea Kaskazini.

Chanzo: RTRE