1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yaonywa juu ya ongezeko la wapinga demokrasia

23 Septemba 2023

Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya Katarina Barley leo hii ametoa onyo dhidi ya kuongezeka kwa vuguvugu la wapinga demokrasia barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/4WjCM
Straßburg EU-Parlament l Katarina Barley (SPD)
Picha: Philipp von Ditfurth/dpa/picture alliance

Akizungumza katika mkutano wa ndani wa chama cha siasa cha "Social Democrats (SPD)", Barley amesema demokrasia na utawala wa sheria haviwezi tena kuchukuliwa kwa namna nyepesi katika Umoja wa Ulaya.Mwanachama huyo wa SPD ameyatolea mfano mataifa kama Hungary akisema halipo tena katika mkondo wa kidemokrasia, na muendelezo kama huo unashuhudiwa Poland. Haki za kidemokrasia pia zinaonekana kupunguzwa Italia.Ili kupatikane ustawi bora wa kidemokrasia barani Ulaya, amesma kunahitaji hatua kwa wingi wapigania demokrasia katika Bunge la Ulaya, kunahitajika demokrasia ya kijamii imara ili kufanikisha maendeleo, sera huria, za kirafiki na zenye msingi wa mshikamano katika Umoja wa Ulaya.