1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gachagua akanusha madai ya ufisadi na kujilimbikizia mali

8 Oktoba 2024

Naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua amesema hatojiuzulu nafasi hiyo licha ya kuwasilishwa hoja bungeni ya kumuondoa madarakani.

https://p.dw.com/p/4lWG2
Kenya | Rigathi Gachagua
Naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua Picha: LUIS TATO/AFP

Akilihutubia taifa kutoka makaazi yake rasmi ya Karen mjini Nairobi, Gachagua ameeleza kuwa atafika bungeni leo Jumanne ili kujitetea.

Kiongozi huyo amekuwa kwenye shinikizo kutoka kwa baadhi ya wanasiasa na hata wananchi wanaomtaka ajiuzulu kutokana na tuhuma zinazomkabili za kujilimbikizia mali kinyume cha sheria, kuihujumu serikali na kutoa matamshi ya kuchochea ukabila.

Soma pia:  Wakenya washiriki mdahalo wa kumuondoa makamu wa rais

Ameeleza kuwa baadhi ya mali zake alizirithi kutoka kwa nduguye marehemu gavana wa zamani wa kaunti ya Nyeri Nderitu Gachagua.

Naibu wa rais huyo amefahamisha kuwa aliitisha mkutano huo na waandishi wa habari ili kutoa utetezi wake kabla ya kuwasili bungeni baadaye leo.