1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yapiga marufuku vituo vinne vya habari vya Urusi

17 Mei 2024

Umoja wa Ulaya leo umevipiga marufuku vituo vinne zaidi vya utangazaji kutopeperusha matangazo yao katika mataifa wanachama wake kwa kile uliokitaja kuwa kuenezwa kwa propaganda kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4g0hF
Gazeti la kila siku la Urusi Sobesednik
Gazeti la kila siku la Urusi Sobesednik Picha: MAXIM SHEMETOV/REUTERS

Umoja wa Ulaya leo umevipiga marufuku vituo vinne zaidi vya utangazaji kutopeperusha matangazo yao katika mataifa wanachama wake kwa kile uliokitaja kuwa kuenezwa kwa propaganda kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine pamoja na habari za kupotosha, wakati ambapo Umoja huo wa unaelekea katika uchaguzi wa bunge ndani ya wiki tatu zijazo.

Vituo hivyo vinajumuisha kituo cha habari cha Voice of Europe, RIA, Novosti, Izvestia na Rossiyskaya Gazeta, ambavyo Umoja huo unadai viko chini ya udhibiti wa ikulu ya Kremlin.Urusi yawapokonya vibali waandishi habari wa DW Moscow

Katika taarifa, Umoja huo umesema kuwa vituo hivyo vinne hasa vinalenga vyama ya kisiasa vya Ulaya wakati wa uchaguzi.

Mwezi uliopita, Ubelgiji ilianzisha uchunguzi kuhusu kile kinachoshukiwa kuwa uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa Juni kote barani Ulaya, na kusema huduma ya ujasusi ya nchi hiyo imethibitisha kuwepo kwa mtandao unaojaribu kudhoofisha uungwaji mkono wa Ukraine.