1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU kuweka vikwazo vipya kwa wazalishaji wa droni Iran

Hawa Bihoga
18 Aprili 2024

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuweka vikwazo vipya kwa ndege zisizo na rubani na watengenezaji wa makombora wa Iran kutokana na shambulio la Tehran dhidi ya Israel mwishoni mwa juma lililopita.

https://p.dw.com/p/4eu0k
Brussel, Ubelgiji | Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel
Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles MichelPicha: Kenzo Tribouillard/AFP/Getty Images

Mkuu wa Umoja wa Ulaya Charles Michel amesema, vikwazo hivyo ni ishara na ujumbe wa wazi kwa Iran na nia ya Umoja huo ni kuyalenga makampuni yanayotengeneza zana hizo. 

Soma pia:Iran yaipa onya kali Israel isijaribu kujibu mashambulizi

Umoja wa Ulaya tayari umeiwekea Iran vikwazo kutokana na usambazaji wake wa ndege zisizo na rubani kwa Urusi kutokana na vita vyake nchini Ukraine, lakini vimekuwa na athari ndogo katika kuzorotesha uhusiano kati ya Tehran na Moscow.