1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

EU kutumia fedha iliyotokana na mali ya Urusi kununua silaha

21 Machi 2024

Viongozi wa Umoja wa Ulaya leo watajadili juu ya mpango wa kutumia mabilioni ya fedha kama faida iliyotokana na mali ya Urusi iliyozuiwa ili kununua silaha na kuipa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4dxON
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen( kulia) akiwa mjini Brussels
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen( kulia) akiwa mjini BrusselsPicha: Virginia Mayo/AP/dpa/picture alliance

Urusi hata hivyo imeulezea mpango huo wa Umoja wa Ulaya kama ujambazi na wizi.

Viongozi hao 27 pia watajadili kuhusu jinsi Umoja wa Ulaya unavyoweza kujilinda zaidi na kuimarisha uwezo wake wa kijeshi wakihofia kuwa uvamizi wa Urusi hautoishia kwa Ukraine.

Soma pia:  Umoja wa Ulaya walaani uchaguzi wa Urusi ndani ya Ukraine

Katika mkutano wa kilele wa siku mbili utakaofanyika mjini Brussels, kando na vita vya nchini Ukraine, viongozi hao pia wataujadili mzozo wa Israel na Hamas, ombi la Bosnia la kujiunga na Umoja huo pamoja na maandamano ya wakulima.

Hata hivyo, ajenda kuu itakuwa vita vya Ukraine huku Rais Volodymyr Zelenskiy akitarajiwa kuhudhuria mkutano huo kwa njia ya video.