Mataifa ya Ulaya lazima yajiandae na ongezeko la joto
13 Machi 2024Kauli hiyo ni baada ya mwaka 2023 kuwa katika rekodi ya kubwa zaidi ya joto zaidi.Akitoa onyo hilo amesema "Ulaya ndilo bara linalopata joto kwa kasi zaidi tangu miaka ya 1980 ambapo ongezeko lake lilikuwa karibu mara mbili ya kiwango cha kimataifa."
Katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Strasbourg, ambapo Bunge la Ulaya lilikuwa na kikao cha mashauriano, Sefcovic na kamishna wa mabadiliko ya tabia nchi wa Umoja wa Ulaya, Wopke Hoekstra waliwasilisha waraka unaotoa mapendekezo kwa nchi wanachamawawa umoja huo ili hatua zichukuliwe.
Pamoja na masuala mengine kadhaa katika mapendekeuo yao kuna suala la ushirikiano bora, kuongeza matumizi ya takwimu na ufuatiliaji na kuwapa wafanyabiashara na watunga sera taarifa bora zaidi ili waweze kupata majawabu.