1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU kuirai Hungary kujiunga nao katika kuifadhili Ukraine

1 Februari 2024

Viongozi wa Umoja wa Ulaya watajaribu kumrai Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban kujiunga na mpango wa kutoa ufadhili kwa Ukraine ila wako tayari pia kuipa Ukraine fedha hizo bila Hungary iwapo watashindwa kumridhisha.

https://p.dw.com/p/4buW1
Brussels, Ubelgiji | Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borell
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep BorellPicha: MOHAMED AZAKIR/REUTERS

Mpango huo unajumuisha kuisaidia Ukraine kuyatimiza mahitaji yake ya kati ya mwaka 2024 hadi 2027 kwa kuipa yuro bilioni 33 kama mkopo na bilioni 17 zengine ambazo haitohitajika kuzilipa.

Fedha hizo zitatoka kwenye bajeti ya Umoja wa Ulaya ili kuiwezesha Ukraine kifedha wakati inapopambana na uvamizi wa Urusi.

Soma pia:EU kuirai Hungary kuhusu msaada kwa Ukraine

Mkutano ulioitwa leo kwa ajili ya suala hilo ndio fursa ya mwisho ya kufikia makubaliano kabla kuuwacha mpango wa kutumia bajeti ya Umoja wa ulaya kama njia ya kuifadhili Ukraine.

Hatua hii ni muhimu wakati ambapo kuna ati ati kuhusiana na ufadhili kutoka Marekani kwa sababu ya mivutano iliyoko katika bunge kuhusu kufadhiliwa kwa Ukraine.