UchumiUlaya
EU kuchukuwa hatua kuelekea euro ya kidijitali
28 Juni 2023Matangazo
Hatua ya kuanzisha sarafu ya kidijitali ya euro ilianza mwaka wa 2020 wakati rais wa benki kuu ya Ulaya Christine Lagarde alipopendekeza wazo hilo na benki hiyo yenye makao yake mjini Frankfurt, Ujerumani ikaanzisha mashauriano ya umma.
Watetezi wa sarafu ya euro ya kidijitali wanasema itajaziliza sarafu taslimu na kuhakikisha Benki Kuu ya Ulaya - ECB haiachi pengo ambalo linaweza kujazwa na watendaji wengi wasiodhibitiwa na wasio wa Ulaya pamoja na benki kuu za mataifa.
Wakosoaji wanahoji uhitaji wa euro ya kidijitali na kuonya juu ya hatari kubwa, huku utafiti wa ECB yenyewe ukibaini kuwa umma ulikuwa na wasiwasi kuhusu ufaragha wa malipo.