ECOWAS kukutana Alhamis kuhusu Niger
7 Agosti 2023Matangazo
Taarifa ya kuitishwa mkutano huo imetolewa na msemaji wa ECOWAS siku moja baada ya kumalizika kwa muda wa wiki moja uliotolewa na jumuiya hiyo kwa wanajeshi nchini Niger kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum.
Soma zaidi: Wanajeshi wa Niger wadai kumuondoa madarakani Rais Bazoum
ECOWAS iliwaonya majenerali wa Niger kuwa wangelikabiliwa na vikwazo vikali vya kiuchumi na uwezekano wa kutumwa kikosi cha jeshi nchini humo iwapo wangelikataa kuondoka madarakani.
Hata hivyo, wanajeshi hao waliopindukia serikali mnamo Julai 26 wamepuuza shinikizo hilo la kikanda na hapo jana walitangaza kuifunga anga ya nchi hiyo kwa muda usiojulikana, kufuatia wasiwasi unaongezeka wa uingiliaji kati kijeshi kutoka nje.