1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dunia yashtushwa na kifo cha Bryant

27 Januari 2020

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amekuwa miongoni mwa watu wa awali mashuhuri waliotuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha nyote wa zamani wa timu ya mpira wa kikapu ya LA Lakers nchini Marekani Kobe Bryant.

https://p.dw.com/p/3WqjK
USA l Ex-NBA-Superstar Kobe Bryant stirbt bei Helikopterabsturz
Picha: picture-alliance/Photoshot

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amekuwa miongoni mwa watu wa awali mashuhuri waliotuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha nguli wa zamani wa timu ya mpira wa kikapu ya LA Lakers ya nchini Marekani Kobe Bryant aliyefarika dunia jana katika ajali ya helikopta.

Obama ameungana na wachezaji wengine nyota wa zamani wa mpira wa kikapu waliowahi kucheza na Bryant enzi ya uhai wake katika ligi ya NBA ya nchini Marekani ikiwa ni pamoja na Shaquille O'Neill, Magic Johnson, Michael Jordan na Kareem Abdul - Jabar.

Bryant 41, amefariki dunia pamoja na binti yake wa miaka 13 Gianna, pamoja na watu wengine saba waliokuwa kwenye helikopta hiyo iliyoanguka katika eneo la Calabasas, jijini Los Angeles.

Mkuu wa polisi jijini Los Angeles Alex Villanueva hata hivyo alikataa kutoa utambulisho wa watu hao wengine hadi uchunguzi wa miili utakapokamilika.

Wanamuziki na washiriki kwenye tuzo za muziki za Grammy pia wametoa heshima zao kwenye uwanja wa nyumbani wa Bryant na LA Lakers wa Staples Center ulioko Los Angeles, masaa kadhaa baada ya taarifa za kifo chake.