Djibouti na Ethiopia mbioni kujiunga na EAC
11 Oktoba 2023Kujiunga kwa mataifa hayo kunatajwa na jumuiya hiyo kuwa ni sehemu ya mkakati wa kufikiwa kwa soko la kibiashara la watu milioni 800.
Japo hajabainisha kama ni lini nchi hizo zitajiunga rasmi, Dr. Mathuki amesema maono ya viongozi wa serikali za nchi wanachama ni kuziunganisha nchiza pembe ya Afrika na kuwa na soko moja kubwa la kibiashara.
Hayo yanakuja huku nchi ya Somalia iliyo upande wa mashariki mwa Afrika ikikamilisha hatua za mwisho za kisheria kabla ya kuidhinishwa kuwa mwanachama mpya wa jumuiya hiyo kongwe barani Afrika.
Soma pia:Somalia yajadiliwa kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki
Kwa sasa Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi saba ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Burundi, Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo iliyojiunga na jumuiya hiyo mwaka mwaka 2022.