Dhuluma dhidi ya watoto zaongozeka Busia
18 Julai 2024Katika maeneo ya barabarani utaona vijana wadogo wanafanya biashara za uchuuzi wa bidhaa mbali mbali hadi migodini.
Soma pia:Nusu ya Wakenya wako kwenye mkwamo wa kifedha - Utafiti
Na kwenye ziwa Viktoria utawaona vijana wakifanya uvuvi wa samaki. Hizi ni miongoni mwa ajira kwa watoto, katika jimbo la Busia ambako viwango vya umaskini vinahusishwa na ongezeko la ajira miongoni mwa watoto.
Kando na umaskini, utafiti ulioendeshwa na shirika la nchini Uholanzi la Terre Des Hommes unaonyesha kuwa, jimbo la Busia linaongoza kwa ajira za watoto ikizingatiwa uwepo wake mpakani mwa Kenya na Uganda, lakini pia dhuluma za kimapenzi na ulanguzi wa binadamu.
Soma pia: Umoja wa Mataifa wachunguza utumwa wa ngono Sudan
Utafiti huo unaonesha kwamba asilimia 45 ya watoto wanaoenda shule wameajiriwa na hata asilimia 55 ya ambao hawaendi shule pia wakiwa wameajiriwa.
Lawama nyingi zimeelekezwa kwa wazazi na walezi kutokana na kuongezeka kwa vitendo hivyo, kutokana na kushindwa kuwajibika ipasavyo kukidhi mahitaji ya msingi.
Wakati takwimu hizi zikiongezeka, serikali ya Kenya imekwishaahidi kuimarisha juhudi za kupambana na visa vya ajira miongoni mwa watoto na kusisitiza watoto kupelekwa shuleni.
Kwa mujibu wa takwimu za shirika la kimataifa la kuwahudumia watoto UNICEF mwaka 2023, watoto wa umri kati ya 5 hadi 17 walihusishwa katika ajira za watoto ambazo zilikuwa hatari kwa afya na ukuaji wao.
Sikiliza: