Umoja wa Mataifa wachunguza utumwa wa ngono Sudan
19 Juni 2024Vita vimeendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja kati ya jeshi la serikali linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na vikosi vya RSF vinavyoongozwa na naibu wake wa zamani, Jenerali Mohamed Hamdan Daglo.
Tume Huru ya Kimataifa ya Kutafuta Ukweli ya Umoja wa Mataifa iliyoanzishwa hivi karibuni imepokea ripoti za kuaminika kuhusu matukio mengi ya unyanyasaji wa kingono yanavyofanywa na pande zinazopigana.
Soma zaidi: UN yaonya uwezekano wa janga la kibinadamu al Fashir
Mkuu wa ujumbe huo, Mohammed Chande Othman, ameliambia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva kwamba wanawake na wasichana wameendelea kukabiliwa na mateso ya kubakwa na magenge, kutekwa nyara na kuingizwa katika ndoa za kulazimishwa.
Kikosi hicho kipya cha uchunguzi cha Umoja wa Mataifa mpaka sasa kimewahoji waathiriwa wapatao 80 wakiwemo wanaume na wavulana.