Dhoruba kali yaupiga mji wa Houston na kuwaua watu wanne
17 Mei 2024Matangazo
Watu wanne wameripotiwa kufariki kufuatia dhoruba iliyosababisha pia uharibifu mkubwa wa majengo na miundombinu kadhaa huko Houston, Marekani ambapo pia kaya zaidi ya laki 900,000 zimekosa umeme. Eneo la kusini-mashariki mwa Texas linashuhudia hali hii kwa mara ya pili mnamo mwezi huu.
Soma: Dhoruba kali yapiga maeneo ya Marekani
Mamlaka ya hali ya hewa ya Houston ilitoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kushuhudia katika kaunti kadhaa mvua kubwa na upepo mkali. Mamlaka ya jiji hilo imewataka raia kusalia majumbani mwao hasa kutokana na kwamba barabara nyingi hazipitiki huku safari za ndege zikisitishwa kwa muda.
Pia, shule kadhaa huko Houston zimelazimika kufungwa leo Ijumaa kutokana na hali hiyo.