1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dhoruba kali yapiga maeneo ya Marekani

2 Aprili 2023

Idadi ya vifo kutokana na dhoruba kali iliyopiga kusini-kati na mashariki mwa Marekani ikiandamana na upepo mkali na vimbunga imepanda hadi watu 22 huku wengine kadhaa wakijeruhiwa

https://p.dw.com/p/4PbW7
USA, Arkansas | Tornado Schäden in Little Rock
Picha: Andrew DeMillo/AP/picture alliance

Msemaji wa shirika la usimamizi wa masuala ya dharura katika jimbo la Tennessee, mojawapo ya majimbo yaliyoathirika pakubwa tangu mvua kubwa zilipoanza Ijumaa, amethibitisha vifo saba vinavyohusiana na hali ya hewa.

Kulikuwa na vifo vya watu 15 vilivyoripotiwa katika majimbo ya Arkansas, Mississippi na Alabama katika upande wa kusini, Indiana na Illinois katika eneo la Kati Magharibi na jimbo la Delaware la Atlantik ya kati.

Gavana wa Arkansas Sarah Huckabee Sanders ametangaza hali ya dharura na kuamuru jeshi la ulinzi wa taifa kusaidia na juhudi za uokozi. Amesema amzungumza na Rais Joe Biden, ambaye ameahidi kuharakisha msaada wa serikali.