1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoItaly

Dawa za kusisimua misuli: Paul Pogba asimamishwa kwa muda

12 Septemba 2023

Kiungo wa timu ya Juventus Paul Pogba amesimamishwa kucheza kandanda kwa muda baada ya kukutwa na kosa la kutumia ya dawa za kusisimua misuli.

https://p.dw.com/p/4WDdE
Paul Pogba | französischer Fußballspieler
Picha: Italy Photo Press/picture alliance

Uamuzi huo umechukuliwa na Mahakama ya kitaifa ya Italia yenye dhima ya kupambana na matumizi ya dawa hizo za kuongeza nguvu mwilini.

Mahakama hiyo imesema Pogba alifanyiwa vipimo baada ya ushindi wa timu yake ya Juventus dhidi ya Udinese kwa mabao 3-0 mnamo Agosti 20 na majibu yalidhihirisha kuwa mchezaji huyo wa Ufaransa ambaye hakushiriki mechi hiyo, alikuwa na viwango vya juu vya homoni ya "testosterone".

Iwapo  Pogba mwenye umri wa miaka 30  atapatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli, anaweza kupigwa marufuku ya kushiriki kandanda kwa muda wa miaka miwili hadi minne. Timu ya Juventus imesema kwa sasa wanatathmini kuhusu hatua zinazofuata.