Colombia yavunja uhusiano na Israel kufuatia vita vya Gaza
2 Mei 2024Rais Petro ameitoa kauli hiyo jana katika mji mkuu wa Colombia-Bogota, wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi na kusisitiza kuwa ulimwengu hautakiwi kukaa kimya.
" Hilo haliwezi kutokea. Hatuwezi kurejea katika nyakati za mauaji ya halaiki, mauaji ya kuwaangamiza watu wote huku tukiangalia bila kuchukua hatua. Ikiwa Palestina itasambaratishwa, basi ubinadamu nao utatoweka." Alisema.
Mnamo mwezi Oktoba, Gustavo Petro alilinganisha vitendo vya jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza na uhalifu uliofanywa na watawala wa kinazi wa Ujerumani.
Soma pia:Waisraeli waandamana kutaka mapigano yasitishwe, mateka warejeshwe
Kujibu kauli hiyo, Israel ambayo ni muuzaji muhimu wa vifaa vya kijeshi kwa Colombia, ilitangaza kusitisha mkataba wa mauzo ya silaha kwa taifa hilo la Amerika Kusini.