Coca-Cola kuwekeza dola bilioni 1 Nigeria
20 Septemba 2024Matangazo
Hayo yameelezwa na Rais Bola Tinubu baada ya mkutano na mkurugenzi na mkuu wa fedha wa Coca-Cola, Zoran Bogdanovic, na maafisa wengine kadhaa wa kampuni hiyo.
Bogdanovic amemwambia Tinubu kwamba tangu mwaka 2013, Coca-Cola imewekeza dola bilioni 1.5 nchini Nigeria ili kutanua uwezo wa uzalishaji, kuboresha ugavi pamoja na kwenye sekta ya mafunzo na maendeleo.
Soma zaidi: Mafuriko yasababisha vifo 30 Nigeria
Nigeria, yenye wakaazi zaidi ya milioni 200 inachukuliwa kama soko muhimu kwa makampuni mengi ya kimataifa, lakini matatizo ya kubadilisha fedha za kigeni, urasimu na mikanganyiko ya sera vimekuwa vikiwakatisha tamaa baadhi ya wawekezaji.