1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China,Tanzania na Zambia zasaini makubaliano mradi wa reli

4 Septemba 2024

Rais Xi-Jinping pamoja na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Zambia, Hakainde Hichilema wamesaini mkataba wa maelewano kuhusu mradi wa reli unaolenga kuimarisha mtandao wa usafiri wa reli na bahari.

https://p.dw.com/p/4kGDi
China Beijing | Mkutano wa Kilele wa China-Afrika| Kusainiwa kwa mkataba kati ya China-Tanzania-Zambia.
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka China, Tanzania, na Zambia wakisaini makubaliano ya ujenzi wa reli ya Tazara, wakishuhudiwa na marais wao mjini Beijing.Picha: Tanzania presidential communication unit

Shirika la habari la China, limeripoti leo Jumatano kwamba China, Tanzania na Zambia zimesaini makubaliano ya mwanzo kuhusu mradi wa reli unaolenga kuimarisha mtandao wa usafiri wa reli na bahari katika kanda ya Afrika Mashariki.

Rais Xi-Jinping pamoja na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Zambia, Hakainde Hichilema wamesaini mkataba huo wa maelewano mjini Beijing ambako viongozi hao wanashiriki mkutano wa ushirikiano kati ya China na Afrika ulioanza rasmi leo.

Soma pia China, Zambia, Tanzania zasaini makubaliano ya ukarabati wa reli

Shirika la habari la China limesema, nchi hiyo iko tayari kuutazama mkutano huo kama fursa ya kupiga hatua mpya ya kufufua ushirikiano wa reli kati ya Tanzania na Zambia ili kuimarisha mtandao wa usafiri wa reli na bahari kwenye kanda hiyo.

Mwanzoni mwa mwaka huu Benki ya Dunia iliidhinisha dola milioni 270 za kusaidia kuimarisha usafiri wa reli kati ya mataifa hayo jirani ya Tanzania na Zambia kunyanyua biashara kwenye eneo hilo.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW