China tuzuwie kuenea mgogoro wa kibinadamu Gaza
20 Novemba 2023Waziri wa mambo ya nchi za nje wa China Wang Yi amewaambia wanadiplomasia wa mataifa ya kiarabu na kiislamu kwamba Jumuiya ya kimataifa ni lazima ichukue hatua kukomesha mgogoro wa kibinaadamu unaoendelea katika ukanda wa Gaza.
Ujumbe wa Mawaziri wenzake kutoka mamlaka ya Palestina, Indonesia, Misri, Saudi Arabia na Jordan wapo ziarani mjini Beijing, kwa mazungumzo yanayonuiwa kuzuwia kutanuka kwa mgogoro kati ya Israel na Hamas.
Amewataka wajumbe wote kushirikiana na China katika kutafuta amani ya Mashariki ya Kati
Soma pia:Israel yatangaza kupanua operesheni zake Gaza
Waziri wa mambo ya nje alisema Leo ni maadhimisho ya miaka 35 tangu yalipoanzishwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya China na Palestina.
kupitia siku hii alitoa wito wa jumuia ya kimataifa kuja pamoja kudhibiti hali Gaza na kurejesha amani ya Mashariki ya Kati haraka iwezekanavyo.
Wang aliongeza kuwa Beijing ni rafiki mkubwa wa mataifa ya kiarabu na ya kiislamu na nchi yake imekuwa ikiunga mkono juhudi za watu wa Palestina za kupata hakina matakwa yao, huku akisistiza kuwa China inasimamia haki na uadilifu katika mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati.