1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yahimiza upatikanaji wa amani Ukraine

Hawa Bihoga
27 Februari 2023

China imesema inatafuta majadiliano na suluhisho la amani kwa Ukraine, licha ya Marekani kuonya kwamba Beijing huenda inazingatia kutoa silaha kwa uvamizi wa mshirika wake Urusi.

https://p.dw.com/p/4O2I5
Deutschland | Münchener Sicherheitskonferez | Wang Yi
Picha: Johannes Simon/Getty Images

China ambayo ilitangaza mafungamano yasio ukomo na Urusi muda mfupi kabla ya uvamizi wa Urusi mwaka mmoja uliyopita, imekataa kulaani uvamizi huo na wiki iliyopita ilichapicha mpango wa nukta 12 unaotoa wito wa kusitisha mapigano na upunguzaji wa hatua kwa hatua wa mzozo kwaa pande mbili.

Macron asema ataitemebelea China kuishinikiza isaidie katika upatikanaji amani ya Ukraine na Urusi

Serikali mjini Kyiv alikaribisha baadhi ya vipengele vya mpango huo, huku ikisisitiza kwamba hakutakuwa na amani hadi Urusi iondowe wanajeshi wake, jambo ambalo Urusi inalikataa.  

Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov, amesema mpango wa China unapaswa kuchambuliwa kwa kina na kuzingatia maslahi ya pande zote, lakini kwa sasa Moscow haijaona ishara za utatuzi wa amani wa mzozo huo.