Rais Macron kwenda China kujadili vita vya Urusi na Ukraine
25 Februari 2023Matangazo
Akizungumza siku moja baada ya China kuomba mazungumzo ya amani kufanyika kati ya pande hasimu huku ikitangaza mipango yake ya kumaliza vita hivyo, Macron amesema amani itapatikana iwapo Urusi itasitisha uchokozi wake, kuondoa wanajeshi wake na kuheshimu uhuru wa Ukraine pamoja na watu wake.
Wafadhili wakutana Paris kusaidia Ukraine
Ameitahadharisha China kutotoa silaha kwa Urusi na kuitaka pia Beijing kuiomba Moscow kutothubutu kutumia silaha za sumu au nyuklia dhidi ya Ukraine.
China ilitoa pendekezo la vipengele 12 la kutafuta suluhu ya kisiasa katika vita vya Urusi na Ukraine, baada ya madai kutoka kwa nchi za Magharibi kwamba, China inafikiria kuipa silaha Urusi madai ambayo imeyakanusha.