Changamoto za kuwahudumia wakimbizi wa Kongo
20 Juni 2023Licha yakuwa kaulimbiu ya mwaka huu inawataka wakimbizi kuwa na matumaini licha ya kwamba wanaishi mbali na makazi yao, baadhi ya wakimbizi wamechukuwa fursa hii kutowa malalamiko kufuatia hali ngumu ya maisha wakidai kwamba tangu siku kadhaa hawajapata chakula toka mpango wa chakula ulimwenguni WFP.
Vita na majanga mojawapo za sababu za wakimbizi
Tangu pale serikali ya Tanzania ilipokusudia kufunga kambi ya Nyarugusi nchini Tanzania, maelfu ya wakimbizi wamevuka ziwa Tanganyika nakufurikia eneo la Lusenda wakitarajia kupewa fursa ya hifadhi katika nchi za ulaya na kazalika.
Kama inavyoonekana, vita na majanga mbalimbali vimesababisha ongezeko la wakimbizi katika baadhi ya maeneo ya Kivu kusini haswa pia katika kambi za Minova zinazopakana na jimbo jirani la Kivu ya kaskazini.
Ukosefu wa misaada
Tume ya kitaifa inayohusika na wakimbizi CNR inatumika kwa ushirikiano na tume ya umoja wa mataifa husika na wakimbizi UNHCR na mpango wa chakula duniani WFP ili kuleta suluhisho kwa madai ya wakimbizi, ila kuna baadhi ya changamoto kushughulikia wakimbizi.
Hafla mbalimbali zimefanyika katika baadhi ya miji ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuadhimia siku hii. Baadhi ya wakimbizi wameitaka serikali kuwahifadhi katika hali inayoshalili.