1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama tawala Canada chasaka mrithi wa Justin Trudeau

7 Januari 2025

Chama cha Kiliberali cha waziri mkuu aliyetangaza kujiuzulu nchini Canada, Justin Trudeau, kinatafuta waziri mkuu mpya.

https://p.dw.com/p/4otUa
Canada I Mkutano wa habari Justin Trudeau
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amejiuzulu kutokana na shinikizo ndani ya chama chake.Picha: Adrian Wyld/AP/picture alliance

Trudeau alitangaza hatua ya kujiuzulu baada ya kuzidi kupoteza uungwaji mkono ndani ya chama chake na nchini kwa ujumla.

Chama cha Kiliberali kinabidi kimtafute kiongozi mpya huku kikikabiliana na vitisho vya rais mteule wa Marekani Donald Trump vya kuweka ushuru mkubwa dhidi ya bidhaa za kutoka Canada.

Soma pia: India, Canada zafukuziana mabalozi katikati mwa mzozo wa kidiplomasia

Kujiuzulu kwa waziri mkuu Trudeau kumekuja miezi kadhaa kabla ya Canada kuingia kwenye uchaguzi. Trudeau mwenye umri wa miaka 53, amesema ataendelea kuwa waziri mkuu  hadi kiongozi mpya wa chama chake atakapochaguliwa.