Chama cha Kijani chaonya udhibiti mipakani kuwa wa kudumu
17 Septemba 2024Matangazo
Lang amesema jana mjini Berlin kwamba hatua kama hizo ni lazima ziwe na uwiano, huku akionyesha wasiwasi mkubwa.
Amesema jeshi la polisi lina watumishi wachache sana kutekeleza hatua hiyo na wafanyabiashara tayari wameelezea wasiwasi wao juu ya kupanda kwa gharama za mnyororo wa ugavi na kuongeza kuwa udhibiti huo hauwezi kuwa wa kudumu.
Kuimarishwa kwa ukaguzi kwenye mipaka ya Ujerumani na Ubelgiji, Denmark, Ufaransa, Luxemburg na Uholanzi kumeibua pia malalamiko kutoka kwa makampuni ya baadhi ya nchi jirani.
Hatua hizo zitaanza kutatumika kwa miezi sita. Na ni sehemu ya mpango wa usalama unaotekelezwa baada ya msururu wa mashambulizi yanayoshukiwa kuwa ya kigaidi na kuibua wasiwasi kuhusu uhamiaji.