1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Ramaphosa: "Tunasaka vyama vya kuunda serikali ya kitaifa"

7 Juni 2024

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza siku ya Alhamisi kwamba chama chake cha African National Congress, ANC kinasaka kuunda muungano mpana wa serikali ya umoja wa kitaifa.

https://p.dw.com/p/4gl0H
Afrika Kusini | Cyril Ramaphosa
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amekiri kwamba chama chake cha ANC kinahitaji ushirika na vyama vingine ili kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, baada ya kikao na maafisa wa ANCPicha: Jerome Delay/AP/picture alliance

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza jana Alhamisi kwamba chama chake cha African National Congress, ANC kinasaka kuunda muungano mpana wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Ramaphosa amesema lengo kuu la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ni kukabiliana na masuala mazito ambayo raia nchini humo wanataka yashughulikiwe. Alisema hayo baada ya mkutano mrefu na maafisa wa chama.

Rais Ramaphosa, alikiri baada ya masaa kumi ya majadiliano na maafisa hao waandamizi, kwamba chama hicho tawala sasa kitahitaji washirika ili kuunda serikali.

Tayari chama hicho kilikuwa kimefanya mazungumzo na vyama vitano, baada ya kushindwa kupata wingi wa kutosha kwenye uchaguzi wa bunge wiki iliyopita.