1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

Chad yasema shambulio lililotibuliwa lilifanywa na walevi

9 Januari 2025

Msemaji wa serikali ya Chad Abderaman Koulamallah amesema shambulio katika ikulu ya rais wa nchi hiyo lililotibuliwa jana Jumatano, lilifanywa na "kundi la watu wasiokuwa na mipango” na waliokuwa wamelewa.

https://p.dw.com/p/4oyUg
Viongozi nchini Chad wasema shambulio lililotibuliwa katika Ikulu lilifanywa na kundi la watu wasiokuwa na mpango na walevi
Viongozi nchini Chad wasema shambulio lililotibuliwa katika Ikulu lilifanywa na kundi la watu wasiokuwa na mpango na waleviPicha: Sunday Alamba/AP/picture alliance

Milio ya risasi ilisikika karibu na ofisi ya rais katika mji mkuu, N'djamena Jumatano usiku huku jeshi likishika doria na kufunga barabara.

Serikali ilisema baadaye kuwa, vikosi vya usalama vilizuia jaribio la kile walichokiita kudhoofisha nchi hiyo ya Afrika ya Kati na kwamba hali kwa wakati huu imedhibitiwa kabisa.

Katika mahojiano kwenye televisheni ya taifa, msemaji huyo wa serikali ya Chad ameeleza kwamba kundi la washambuliaji 24 waliokuwa na visu na mapanga na waliokuwa walevi, walijaribu kuivamia ikulu ya rais.

Amesema kuwa, washambuliaji hao waliwavamia walinzi wanne waliokuwa kwenye lango la ikulu, na kumuua mlinzi mmoja na kuwajeruhi wengine wawili.