Mataifa kadhaa yajiunga na kesi ya mauaji ya Myanmar
17 Novemba 2023Matangazo
Mataifa hayo yamewasilisha tamko la pamoja la kuingilia kati kesi hiyo katika mahakama hiyo ya kimataifa ya Haki (ICJ). Nchi hizo zimetaja masilahi yao ya pamoja kutaka mkataba wa mwaka 1948 wa kuzuia mauaji ya halaiki na kuadhibiwa kwa uhalifu huo kuzingatiwa.
Kiongozi wa Myanmar asema uasi unatishia kulisambaratisha taifa
Tania von Uslar, afisa wa mambo ya nje wa Ujerumani amesema kupitia ukurasa wake wa X kwamba wanaangazia haswa ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Ujumbe wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa ulihitimisha kuwa kampeni ya jeshi la Myanmar ya mwaka 2017 iliyowafukuza Warohingya 730,000 waliokimbilia nchi jirani ya Bangladesh ilikuwa imejumuisha "vitendo vya mauaji ya kimbari".