Burundi yaomba msaada kukabiliana na athari za mvua
18 Aprili 2024Matangazo
Umoja wa Mataifa umeitaja Burundi kuwa miongoni mwa nchi 20 zilizo katika hatari kubwa ya kukabiliwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, wakati mvua isiyo na kikomo tangu mwezi Septemba mwaka jana ikiendelea kuuharibu mji mkuu wa Bujumbura.
Soma zaidi: Burundi yahitaji msaada kukabiliana na mafuriko makubwa
Eneo la Afrika Mashariki limekuwa likikumbwa na mvua kubwa katika wiki za hivi karibuni ambazo zimegharimu maisha ya takriban watu 58 nchini Tanzania tangu kuanza kwa mwezi huu, huku wengine 13 wakifariki nchini Kenya.