SiasaBurundi
Burundi yaishtumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi
30 Desemba 2023Matangazo
Burundi imesema kundi la waasi la RED-Tabara lilifanya shambulio Desemba 22 karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na kuuwa watu 20, wakiwemo wanawake na watoto.
Soma pia: Shambulizi la waasi lasababisha vifo vya watu 20 Burundi
Akizungumza katika mkutano uliotangazwa na vyombo vya habari vya Burundi kutokea mashariki mwa Burundi, Rais Ndayishimiye alisema makundi hayo ya waasi yamepewa hifadhi, chakula, ofisi na fedha kutoka nchi inayowakaribisha, na kuitaja Rwanda.
Ndayishimiye ameapa kupambana dhidi ya kundi hilo kwa nguvu zote. Hata hivyo kundi hilo na serikali ya Rwanda walikanusha madai hayo.