SiasaBurkina Faso
Burkina Faso yafungia mashirika zaidi ya habari ya kimataifa
29 Aprili 2024Matangazo
Miongoni mwa mashirika yaliotajwa katika agizo hilo la wikendi ni gazeti la Ufaransa Le Monde, gazeti la Uingereza The Guardian, Deutsche Welle ya Ujerumani nakituo cha televisheni cha Ufaransa TV5 Monde.
Vyombo vingine vya habari vilivyotajwa katika agizo hilo ni gazeti la kikanda la Ufaransa la Ouest-France, APAnews na Agence Ecofin.
Soma pia: Burkina Faso yasitisha matangazo ya redio ya BBC na VOA kutokana na kutangaza mauajiSiku ya Alhamisi CSC ilitangaza kuwa imeagiza kampuni za huduma za mtandao wa intaneti kukatiza huduma zake kwa wiki mbili kwa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC na lile la Marekani la Voice of America, VOA kwa kuiangazia ripoti hiyo ya HRW.