1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Afrika Mashariki inaweza kuwa na viwango sawa vya kodi?

13 Machi 2024

Wataalamu wa biashara na uchumi katika eneo la Afrika mashariki wamepongeza hatua ya bunge la jumuiya hiyo EALA kupitisha muswaada wa kusawazisha sheria za kodi na ushuru katika kanda hiyo ya kiuchumi.

https://p.dw.com/p/4dTpC
Kenya Nairobi 2023 | Gikomba
Wakaazi wa Nairobi katika soko la GikombaPicha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Spika wa bunge la EALA Joseph Ntakirutimana amefahamisha rasmi kuwa muswaada wa kusawazisha sheria za kodi afrika mashariki umepitishwa kwa maridhiano ya pamoja.Bunge la Kenya lapitisha muswada tata wa fedha

Kwa mujibu wa muswaada huo uliowasilishwa kwenye kikao cha bunge la EALA mjini Nairobi, mataifa ya jumuiya ya afrika mashariki yatatakiwa kusawazisha sheria zao za kodi na ushuru hasa kuhusiana na viwango.

Kwa mfano kiwango cha kodi ya ongezeko la thamani maarufu kama VAT kimependekezwa kuwa sawa katika mataifa yote.

 Kenya, Nairobi | M-PESA
Miamala ya kwenye simu kupitia M-pesa Picha: Daniel Irungu/EPA/dpa/picture alliance

Kwa sasa kila taifa lina kiwango chake kati ya asli mia 15 hadi 18. Kwa namna hii, mwekezaji au mfanyabiashara kutoka nchi moja anapata wepesi wa kuendesha shughuli zake katika nchi nyingine kwa gharama ile ile pamoja na kwamba sera na taratibu za kukadiria malipo husika zinasawazishwa pia.Mawaziri Tanzania kujadili sakata la tozo ya miamala

Wakati wa kujadili muswaada huo wabunge kadhaa walitoa hoja zao wakiunga kupitishwa kwake kwa kusema. 

Wataalamu wa uchumi na biashara wamepokea habari hizo kwa furaha wakisema kuwa hii itakuwa muhimu katika kuinua kiwango cha biashara na uwekezaji si tu miongoni mwa mataifa hayo lakini pia kwa wale kutoka mataifa mengine ambao wanavutiwa na soko la pamoja la kanda hiyo. Kwa sasa biashara miongoni mwa nchi hizo ni kwa asli mia 15 na wataalamu wanatarajia kitastawi kwa zaidi ya asli mia 40.

Watanzania walalamika juu ya ongezeko la bei ya mafuta

Dkt Julius Byaruhanga ni msomi wa sera za uchumi na biashara na pia mshauri wa sekta binafsi na ametoa tathmini yake akisema kwamba "napongeza hatua hii kwani sasa bidhaa za afrika mashariki zitashindana vilivyo na zile kutoka mataifa ya kigeni."Tanzania yasema makusanyo ya kodi bado yako chini

Muswaada husika ambao umejadiliwa kwa miaka kadhaa miongoni mwa wadau katika sekta binafsi Afrika Mashariki unanasibishwa na sheria ya biashara katika Umoja wa Ulaya. Hii ndiyo hurasisha shughuli za biashara miongoni mwa mataifa hayo na raia wa kila nchi hunufaika kwa kununua bidhaa kwa bei zinazokaribiana. Mkurugenzi wa baraza la wafanyabiashara afrika mashariki EABC John Bosco Kalisa aliambia hivi DW kwa njia ya simu kuwa "tunapokea kwa furaha hatua hii kwani sasa sheria itaondoa hali ya ushindani usiostahili  na kuleta usawa miongoni mwa wafanyabiashara."Kodi mpya ya miamala Tanzania yawatia wananchi wasiwasi

Ila mashaka ya wadau katika sekta binafsi pamoja na wasomi ni kwamba huenda mataifa fulani yatasita katika kuitikia utekelezaji wa sheria husika ndani ya mipaka yao. Hii ni kutokana na hali ambapo mara kadhaa mataifa hayo yamewekeana vizingiti visivyo vya kodi kama vile kupiga marufuku kwa bidhaa za nchi nyingine kuingizwa nchini mwao.