1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Bunge la Brazil lasema Bolsonaro atakiwa kujibu mashitaka

Josephat Charo
18 Oktoba 2023

Kamati ya bunge la Brazil imebaini kuwa rais wa zamani Jair Bolsonaro anatakiwa kujibu mashitaka ya jaribio la mapinduzi kwa wafuasi wake kuishambulia ikulu ya rais, mahakama ya juu na makao makuu ya bunge mwezi Januari.

https://p.dw.com/p/4Xfc7
Brasilien Brasilia | Prozess gegen Jair Bolsonaro
Picha: EVARISTO SA/AFP/Getty Images

Kamati iliyokuwa inachunguza maandamano ya machafuko ya Januari 8 katika mji mkuu Brasilia imekamilisha kipindi cha miezi mitano cha kusikilizwa kwa kesi hiyo kwa kutoa ripoti inayopendekeza waendesha mashitaka pia wamfungulie mashitaka Bolsonaro kwa kujaribu kuupindua utawala wa sheria, kusababisha machafuko ya kisiasa na kuhusika katika njama ya kufanya uhalifu.

Soma zaidi: Bolsonaro achunguzwa kwa ufisadi wa dola 70,000

Ingawa kisheria ripoti hiyo haimlazimishi mwendesha mashitaka mkuu achukuwe hatua, lakini ndiyo mpya katika mfululizo wa masaibu ya kisheria yanayomkabili Bolsonaro ambaye tayari anachunguzwa kwa madai mbalimbali ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.