Bolsonaro achunguzwa kwa ufisadi wa dola 70,000
12 Agosti 2023Mapema hivi leo, maafisa wa polisi walivamia nyumba na ofisi za watu kadhaa wanaotuhumiwa kuhusika na mkasa huo, akiwemo jenerali mmoja wa juu jeshini. Mwenyewe Bolsonaro amekana kufanya kosa lolote kuhusiana na zawadi hizo. Afisa mmoja wa polisi ameliambia shirika la habari la AP kwamba wameomba ruhusa ya mahakama kuchunguza akaunti binafsi za benki na taarifa za fedha za Bolsonaro, na pia msaada wa shirika la ujasusi la Marekani, FBI.
Soma zaidi: Polisi wachunguza vito vya thamani vya Bolsonaro vilivyoingizwa Brazil
Kesi hii ni sehemu tu ya kesi nyengine kadhaa, ambazo rais huyo wa zamani wa Brazil anachunguzwa. Tayari anakabiliwa na uchunguzi juu ya ushiriki wake kwenye uvamizi uliofanywa na wafuasi wake dhidi ya mji mkuu na taasisi za serikali kupinga kushindwa kwake kwenye uchaguzi na kutangazwa kwa hasimu wake, rais wa sasa, Lula da Silva.