Chama cha BSW chapinga Ujerumani kuipa Ukraine silaha
3 Novemba 2024Hali hii inaongeza mvutano katika serikali kuu ya mseto inayoongozwa na Kansela Olaf Scholz, ikihatarisha msaada wa Ujerumani kwa Ukraine.
Chama cha SPD cha Scholz jimboni Brandenburg kimeunga mkono taarifa ya kupinga silaha pamoja na BSW, lakini chama cha Kijani kimeonya kuwa kusitisha msaada kunaweza kuhatarisha usalama wa Ujerumani.
Wagenknecht anasisitiza kuingiza sera za kupinga vita katika miungano ya majimbo, mnamo wakati mabadiliko ya maoni ya umma yakionyesha kupungua kwa shauku ya kuiunga mkono Ukraine.
Soma pia:Wapiga kura katika jimbo la Brandeburg wanashiriki uchaguzi muhimu
Hata hivyo, BSW inakabiliwa na migogoro ya ndani kutokana na msimamo mkali wa Wagenknecht, ambao unayumbisha umoja wa chama.
Katika jimbo la Thuringia, kiongozi wa BSW, Katja Wolf, alikosolewa kwa kupunguza makali ya msimamo wa chama, na wachambuzi wanaonya kuwa masharti makali yanaweza kuhatarisha uimara wa muda mrefu wa BSW.